Monday, April 28, 2008

SWAHILI

2857 - Swahili

YANIPASA NIFANYE NINI NIPATE KUOKOKA?

J.D. Phillips

1. MWAMINI Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako (Matendo 16:30,31). Lakini pasipo imani haiiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yoko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao (Waebrania 11:6). Aaminiye na kubatizwa ataokoka (Marko 16:16). Sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu (Yohana 8:24). Hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake. Yakobo 2:17).

2. TUBUNI mkabatizwe kila mmoja jina lake Yesu Kristu (Matendo 2:38). Lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo (Luka 13:3,5). Mungu ... sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu (Matendo 17:30). Mungu amewajalia hata mataifa nao toba liletalo uzima (Matendo 11:18).

3. Kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu (Warumi 10:10). Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu (Warumi 10:9). Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni. (Mathayo 10:32). Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu akiye hai. (Mathayo 16:16). Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu (Matendo 8:37).

4. UBATIZO, unaowaokoa ninyi pia siku hizi (1 Petro 3:21). Aaminiye na kubatizwa ataokoka (Marko 16:16). Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu (Yohana 3:5). Kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu (Tito 3:5). Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu (Matendo 2:38). Simama, ubatizwe, ukaoshe dhambi zako (Matendo 22:16). Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo (Wagalatia 3:27). Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? (Warumi 6:3). Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya (2 Wakorintho 5:17).

5. TUPATE KUISHI KWA kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema. (Tito 2:12-14).

Nanyi mmeyashika yale mapokeo vile vile kama nilivyowatolea. (1 Wakorintho 11:2).

Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi nyote. Amina. (Ufunuo 22:21).

Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake. (Ufunuo 22:14).

Amina; na uje, BwanaYesu!

-----------------------------------------------------------------

2866 - Swahili

Akasema, Nitawezaje Kuelewa?

Matendo 8:26-40

26. Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka ukaende upande wa kusini hata njia ile itelemkayo kutoka Yerusalemu kwenda Gaza; nayo ni jangwa.

27. Naye akaondoka, akaenda; mara akamwona mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi, aliyewekwa juu ya hazina yake yote;

28. Naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu, akawa akirejea, ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya.

29. Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukashikamane nalo.

30. Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je!

31. Yamekuela haya unayosoma? Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye.

32. Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili, Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake amkataye manyoya, Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake.

33. Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa. Ni nani atakayeeleza kizazi chake? Kwa maana uzima wake umeondolewa katika nchi.

34. Yule tswashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba, nabii huyu asema maneno haya kwa habari ya nami; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine?

35. Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu.

36. Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; Ni nini kinachonizuia nisibatizwe?

37. Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.

38. Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote mawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza.

39. Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashiasimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi.

40. Lakini Filipo akaonekana katika Azoto, na alipokuwa akipita akahubiri Injili katika miji hata akafika Kaisaria

No comments: